Download Mbuzi Mp3 Audio by Dizasta Vina
Here’s an amazing song and music lyrics from the talented Tanzanian rapper and record producer, “Dizasta Vina“. It’s a song titled “Mbuzi“, and was released in 2024. This beautiful song, accompanied by a stunning music video, audio, and lyrics, is sure to captivate listeners of all ages. Don’t miss out on this beautiful musical experience.
Get MP3 audio, Download, Stream, and Share this powerful song with your friends and family, and let the blessings overflow! By sharing it with your loved ones, you’re spreading the goodness and joy that this song brings. #CeeNaija
Lyrics: Mbuzi by Dizasta Vina
Mbuzi alipata wadudu kwenye kwato
Iliathiri furaha na nguvu alizonazo
Mchungaji alihakikisha mbuzi ananawa
Aliondoa wadudu wote kisha akamweka dawa
Alikampangusa chawa akampa chakula kwa wakati
Akamjengea chumba kwa nafasi
Ajisikie huru, Akashika ratiba na itifaki
Muda ukapita afya mbuzi ikatamalaki
Mtaa ikahamaki ukasukwa uvumi
Kuwa bwana Kheri Anatoa muda kisha sumni
Japo hali yake ya uchumi ilikuwa ni duni
Aliuza matunda mboga chache na kuni
Hakuna siku mbuzi alipiga kelele kwa njaa
Watu walimwonea gere balaa
Alinawiri kwa kilele cha umaridadi
Majambazi walipiga misele kadhaa
Na usiku hauwi mwanana akisikia mbiu
Mbuzi akilalama kwamba anahisi kiu
Mchungaji alikuwa macho, Akatambua kuna
Magonjwa nyemelezi akavumbua chanjo
Mbuzi aling’ara alinona
Manyoya yalitawala kuashilia afya kila kona
Hakuwepo hata mwanga mmoja wa kuroga
Hata Waliojaribu kuchanja walikoma
Najiuliza maana ya upendo nini
Mpaka uwe na kingi ndio ushee?
Au pesa kipindi michango ya sherehe?
Au mzazi anayetamani uendelee?
Ndio maana anakulea ile umlee
Inasadikika kuwa upendo wa kweli ni kujali
Mama mzazi homa ikikushika tu halali
Tabasamu analokupa unaposhika Masarali
Ungekuwa hai ingekuwa kutoa mimba ni halali?
Wazalendo wanahitaji hela na nyadhifa
Wanalipwa kutetea sera za taifa
Wadini wanakumbatia itikadi na imani yao
Mpaka wanamwaga damu wenzao
Au mapenzi kwenye timu inapoingia mtimani
Unaumia inashika mkia na hauhami
Kufichiana dhambi tabia wanayoisifia masela
Au mjeshi anavyofia bendera
Nani anajua siri ya kupenda penda?
(Ni) kujitoa sadaka kwa ajili ya mwenza?
Wapo wanaosema kuwa kupenda ni ushupavu
Wanaumizwa wanachukia wanaandika vitabu
Ukijua mwenza wako ana mtu anampenda
Utampa nafasi aende upige moyo konde?
Mama akifariki na una dawa ya kusahau maumivu
Swali ni utakula vidonge?
Je upendo wa kweli ni mpaka aagize mungu?
Aliyesema ufuge paka alafu umchinje kuku
Amemmtoa mwanaye kama mdhamini msalabani
Awafie watu ambao dini hazifanani
Bado Mawazo yananisumbua nasinzia
Nawaza ingekuwaje tungechagua familia
Je mtoto angempenda baba angekuwa lofa?
Au Baba angemchagua mtoto angejua ni shoga?
Wanandoa tungekuweka kwenye Time Chamber
Muda urudi ungemchagua patner wako tena?
Wangapi wanawish wangepita sehemu hii?
Wangapi wangemchagua Justin Bieber na Jay Z?
Kabla ndoa haijakufunga pini
Jiulize kama mkeo angekuwa na wewe ka’ ungekuwa chini?
Licha ya hizi nyimbo zinazofanya watu walie sana
Washikaji walingoja niwe msanii ndio niwe mwana
Pengine inabadili maana ya upendo
Na kuacha swali upendo je ni haja au matendo?
Mchungaji alifuga mbuzi alifuga na ajenda
Alimjali lakini si kwa sababu alimpenda
Kwani ilipofika sikukuu alitoa vitu
Sufuria jungu kuu akanoa visu
Yule mbuzi mzuri aliyenona sana
Ndiye aliyechinjwa na adhuhuri alichomwa nyama