Top Christian Songs Joel Lwaga – Wadumu Milele

Joel Lwaga – Wadumu Milele

Joel Lwaga Wadumu Milele

Download Wadumu Milele Mp3 by Joel Lwaga

The renowned African Christian music minister, praiser, and worship leader whose songs have blessed lives “” birth out a song of praise worship which he titles “Wadumu Milele“.

Get Audio Mp3, Stream, Share, and be blessed.

DOWNLOAD HERE

Lyrics: Wadumu Milele by Joel Lwaga

Msimamizi wa mipaka ya bahari
Utunzaye ghala ya mvua
Waamua vita ya jua na mwezi
Upepo na mawimbi vyakujua
Uketie mahali pa siri
Patakatifu palipo inuka
Wautangaza mwisho mwanzoni
Hakuna usilo lijua
Nani wa kulinganishwa nawe Jehova mwenye nguvu

Ufalme wako ni wa zamani zote vizazi vyote
Miaka kwako sio umri (miaka kwako sio umri)
Vizazi kwako si ukomo (vizazi kwako si ukomooo)
Miaka kwako sio umri (miaka kwako sio umri)
Vizazi kwako si ukomo (vizazi kwako si ukomo)
Mmh, wadumu milele (wadumu mileleee)
Wadumu milele (wadumu mileleee)
Bwana wadumu milele (wadumu mileleee)
Eh, wadumu milele (wadumu mileleee)

Wewe Bwana ni kama maji
Maji yenye kina kirefu
Maji yenye kina kirefu
Kamwe hayapigi kelele

Ni kweli kuna mabwana wengi
Lakini wewe ni Bwana wa mabwana
Ni kweli kuna miungu mingi
Lakini wewe ni Mungu wa miungu

Siku kwako sio vipindi
Majira kwako sio ishara
Ufikiwi kwa mnara wa Babeli
Jina lako ni ngome imara aah

Nani wa kulinganishwa nawe Jehova mwenye nguvu
Ufalme wako ni wa zamani zote vizazi vyoteee
Nani wa kulinganishwa nawe Jehova mwenye nguvu
Ufalme wako ni wa zamani zote vizazi vyoteee

Miaka kwako sio umri (miaka kwako sio umri)
Vizazi kwako si ukomo (vizazi kwako si ukomo)
Miaka kwako sio umri (miaka kwako sio umri)
Bwana vizazi kwako si ukomo (vizazi kwako si ukomo)

Wadumu milele (wadumu milele)
Umejawa nazo siku nyingi (wadumu milele)
Mwanzo na Mwisho viko ndani yako (wadumu milele)
Umeshiba siku na utajiri (wadumu milele)
Wadumuu milele eeh (wadumu milele)
Eeh, wadumu milele (wadumu milele)
Bwana wadumu milele (wadumu milele)
Bwana wadumu milele (wadumu milele)

Say yeah (yeah)
Yeah (yeah)
Yeah (yeah)
Yeah (yeah)

Say yeah (yeah)
Yeah (yeah)
Yeah (yeah)
Yeah
Nani wakulinganisha nawe, Jehova mwenye nguvu
Ufalme wako ni wa milele yote Bwana

Comment below with your feedback and thoughts on this post.